
Polisi
walijua kabisa msafara wao utakua umewabeba watuhumiwa waliokamatwa
kwenye mafunzo ya kijeshi ambayo yalikua yanatolewa kupitia CD za Al
Qaeda na Al Shabaab hivyo wakajiandaa kwa ukubwa huu
Mwanzoni walikua wamekamatwa 11 tu lakini taarifa nyingine zilizoifikia millardayo.com zinaamplfy kwamba idadi imeongezeka baada ya wengine wawili kukamatwa kulekule walikokamatiwa wengine ambapo hawa wawili hawakukutwa na silaha wala kingine chochote kama ilivyotokea kwa wale wa mwanzo ambao walikutwa na mapanga, silaha mbalimbali pamoja na CD za DVD ambazo zinamafunzo ya kijeshi ya Al Shabaab na Al Qaeda.
Wawili hawa wamekiri kwamba mwalimu wao kule msituni alikua akiwapa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo kupiga karate, utumiaji wa silaha ambapo pia walikua wakiishi hukohuko msituni kwenye Mapango.







