Taarifa zilizotufikia
katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu
cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na
majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation”
zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao
na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni
hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na
majambazi kuanza safari yao.
Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate
hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua
kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya
kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa
kupelekwa Hospitalini.
Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa
Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize
mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na
ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa
mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka
sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka,
Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA
wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na
kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. Endelea kufuatilia
katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha
Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali na tukio hilo, pia
kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi
karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo
ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya
Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.