WAKATI
maadhimisho ya miaka 13 ya Kikosi cha Mizinga inatarajiwa kufanyika leo
kwenye ukumbi wa New Msasani Club, kiongozi wa kundi hilo, Karama
Masoud 'Kalapina' amefichua kumaliza 'bifu' lake na Chid Benz na
kumtangaza kwamba ni miongoni mwa wasanii watakaonegesha onyesho hilo
kabambe.
Aidha Kalapina amesema kuwa makundi na msanii yeyote ambaye
angependa kujitokeza kushiriki katika show yao hata kama siyo kwa
kupanda jukwaani anawakaribisha kwa nia ya kufanikisha maadhimisho hayo
na pia kutangaza Amani na Upendo Tanzania.
Akizungumza mapema asubuhi
hii, Kalapina alisema Chid Benz naye atakuwepo katika show yao, licha
ya kwamba mapema mwezi uliiopita walitibuana baada ya Benz kuvamia shoo
ya Kikosi na kulazimika kutimuliwa jukwaani kitemi na kuibua hisia
kwamba 'vita' ya wawili hao imeanza.
Hata hivyo, Kalapina alisema kwa
sasa kikosi wamekuwa na hivuo wamezika tofauti zao za zamani na kuamua
kufanya kazi baada ya kutumia muda mwingi kufanya harakati za
kuisimamisha hop hop Bongo ambapo ilikuwa ikipata vikwazo vingi kiasi
cha kutotangazika licha ya msaada mkubwa kwa jamii
"Tumeshakuwa,
mambo ya ubabe na kila lililokuwa likiwaudhi watu kwa sasa bhaaas,
ndiyo maana Chid mdogo wangu nimemualika na pia naruhusu makundi yote
yanayotuunga mkono na wasanii wengine waje ukumbini kutuopa sapoti kwa
nia ya kutangaza amani na upendo kupitia tamasha hili la leo," alisema.
Kikosi
cha Mizinga kitafanya onyesho hili likisindikizwa na wasanii kibao
nyota nchini akiwemo 'Dume la Simba' Afande Sele, Manzese Crew, gangwe
Mob, Mansu-Lee, Stereo, Nikki Mbishi, Young Killer na wengine huku
kukiwa na maonyesho mbalimbali yenye utamaduni wa hip hop kama uchoraji
kudance na mengine kibao.