
Hadi sasa waokoaji wamepata miili 8 kutoka ndani ya mgodi huo na bado kuna mfanyakazi mmoja hajapatikana kutoka kwenye huo mgodi wa Doornkop ambao upo Magharibi mwa Johannesburg.
Wachimbaji nane walipatikana wakiwa hai katika chumba kimoja chini ya ardhi ambako walijificha ili kuepuka hayo mawe na moto ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana.