Friday, November 15, 2013

Prof.MUHOGO AMESEMA WANAOSEMA MIKATABA YA MADINI NI YA SIRI HAO WOTE NI WAVIVU WAKUSOMA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.PICHA|MAKTABA 

Awataka kuacha kulalamikia vitu ambavyo havina ukweli, zaidi wajikite kusoma.

Dar es Salaam.Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amechachamaa na kusema hakuna usiri katika mikataba ya uchimbaji madini kati ya Serikali na kampuni. Profesa Muhongo alisema ipo wazi kwa Mtanzania yeyote anayetaka kuiona.
Alisema wanaodai kwamba mikataba hiyo ni siri, ni wavivu wa kusoma na wanazungumza mambo ambayo hawana uhakika nayo.
Profesa Muhongo alisema hayo baada ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Doyosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza kutamka kuwa kuna usiri katika mikataba ya madini na kwamba, suala hilo linahitaji kupatiwa ufumbuzi.
Waziri Muhongo alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo ulioandaliwa na taasisi mbalimbali, zikiwamo HakiMadini na Policy Forum.

“Mikataba yote ipo pale wizarani siyo suala la siri, anayetaka tuondoke naye sasa hivi akaipitie, tatizo letu kubwa ni kwamba Watanzania wengi ni wavivu wa kusoma, wanazungumza tu bila kusoma,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema licha ya mkutano huo kuzungumzia madini, ukiwauliza waliosoma sheria mpya ya madini utakuta wachache.
“Watu wanawalaumu viongozi masuala lakini wanayolaumu hawana uhakika nayo, tukijite zaidi katika kusoma vitu,” alisema.
Profesa Muhongo alisema iwapo watu watasoma sheria na machapisho mbalimbali, malalamiko hayo yataondoka.