Friday, November 15, 2013

HUYU NDO SHABIKI WA KWELI NI BAADA YA KUPUNWA NYUMBA KWENYE KAMALI YA MECHI YA MAN U NA ARSENAL

EmiratesStadFansL_
Arsene Wenger anaweza kuwa hana machungu sana baada ya Arsenal kufungwa na Manchester ukifananisha na shabiki wa Arsenal Henry Dhabasani ambaye hivi sasa hana nyumba baada ya kucheza kamari na kuipoteza nyumba hiyo huko Uganda.
Shabiki wa Manchester united Rashid Yiga aliweka gari pamoja na mke wake huku bwana Henry aliweka nyumba na kila mmoja wao akiamini timu yake itashinda mechi hiyo kwenye ligi ya Uingereza. Kamari hii ilikuwa serious kiasi kwamba waliandikishiana makaratasi mbele ya viongozi wa mtaa na mashahidi walikuwa mashabiki wa timu hizo mbili.
Ripota wa Ugandan Observer amesema kwamba baada ya mechi kuisha alimshudia shabiki huyo wa Arsenal akizimia akijua kwamba amepoteza nyumba yake ambapo ana watoto watano na wake watatu. Shabiki huyo wa Arsenal alitolewa kwenye hiyo nyumba jumatatu baada ya mashabiki wa Manchester united kwenda kuizunguka nyumba yake.