Makamu
wa Raisi Mh Dk Mohamed Gharib Bilal ambae pia alikua Mgeni rasmi katika
Hafla ya Usiku wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF Tanzania kwa
kushirikiana na Montage Limited na Benki M akipokea mfano wa Hundi
yenye Thamani ya Shilingi Milioni 25 za Kitanzania kutoka Kwa Mwakilishi
wa Benki ya NBC kwaajili ya MChango wao katika Kampeni ya Stand up For
Tanzania Mother ambayo inalengo la kukusanya pesa kwaajili ya Kusomesha
wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto
Mgeni
Rasmi Ambaye pia Ni Makamu wa Raisi Wa Tanzania Mh Dk Mohamedi Gharib
Bilal akitoa Vyeti vya kushukuru kwa wawakilishi wa Makampuni yaliyoweza
kudhamini usiku huo wa Chakula cha Hisani ulioandaliwa na AMREF
Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M hafla
iliyofanyika jana Usiku katika Hotel ya Serena
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited Bi Teddy Mapunda akitoa shukrani kwa
Wadhamini na wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla
ya Usiku wa Chakula cha Hisani uliofanyika Jana katika Hotel Ya Serena
ikiwa na Lengo na kutafuta pesa kwaajili ya Kusomesha Wakunga ili kuweza
kusaidia katika kupata wakunga ambao Watatoa huduma na kupunga Vifo vya
Mama na Mtoto hafla hiyo iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa
kushirikiana na Montage Limited na Bank kupitia Kampeni ya AMREF iitwayo
Stand Up for Tanzania Mother iliyozinduliwa mnamo tarehe 15 Mei 2013.
Mwenyekiti
wa Benki M ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mh Nimrodi Mkono
Akitoa neno kwa wageni waalikwa katika Hafla ya Usiku wa Chakula cha
Hisani kwaajili ya kuchangisha pesa ya kusomesha wakunga, Hafla
iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jana Usiku Huku ikiwa imeandaliwa
na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage na Benki M kupitia Kampeni
ijulikanayo Stand Up for Tanzania Mothers
Mmoja
wa Wanafunzi wa Masomo ya Ukunga Kutoka Katika Jamii ya Wafugaji kutoka
Kilindi Bi Tanioi Moringe Akitoa shukrani zake za dhati Kwa AMREF
Tanzania ambao ndio Wameweza kumdhamini Kumsomesha Katika Chuo Cha
Ukunga.