Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana akinywa kahawa huku
Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi ndugu Nape Nnauye katikati
akimiminiwa kahawa kwenye kikombe katika kijiji cha Budalabuhega.
Kikundi
cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu
Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Budala Budalabuhega leo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Abdulrahman Kinana akipita mbele ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kanadi wilayani Itilima.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua bweni la
wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kanadi huku akiongozwa na mkuu wa
shule hiyo Mwalimu Samuel George.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa kahawa
mara baada ya kukaribishwa na wananchi katika kijiji cha Budalabuhega
wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha chama na kuhimiza
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi katika wilaya ya
Itilima mkoa mpya wa Simiyu jana ambapo amekagua miradi mbalimbali na
kuzngumza na wenyeviti wa matawi na mashina katika vikao vya ndani ikiwa
ni pamoja na kufungua mashina, kesho ataendelea na ziara yake katika
jimbo la Bariadi mjini.
Hili ni jengo la zahanati ya kijiji cha Nangale kata ya Ndololezi Kinana alilikagua pia.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na
mganga mkuu wa Zahanati ya Nangale Dk. Kerenge Nyawawa wakati
alipotembelea na kukagua jengo la zahanati hiyo.
Huu
ndiyo uhalisia wa maisha mtoto huyu ambaye hakufahamika jina lake akiwa
amembeba mdogo wake huku akiwa amemshika mkono mwingine katika moja ya
vijiji tulivyopitia katika ziara wilayani Itilima.
Mwenyekiti
wa kikundi cha wafanyabiashara wa mazao katika kata kijiji cha
Mwanihunda Kata ya migato Bw, Michael Ntulugwa akitoa maelezo kwa Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokagua
ghala hilo la kuhifadhia chakula lililojengwa kwa msaada wa World
Vision.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akiwa
amekaa kwenye kigoda wakati alipofika kwenye shina namba 15 Shuleni Kata
ya Migato, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana watatu kutoka
kushoto aliyekaa akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu Ndugu Pascal Mabiti
wakati alipokuwa akiongeza na wananchi katika kata ya Migato.
Wana
CCM wa kata ya Migato wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza nao katika shina
namba 15 shuleni kata ya Migato.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na
Mwenyekiti wa wa shina namba 15 Bwana Michael Sama wakati akiwa katika
shina hilo kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa shina hilo jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea Fedha
Taslimu shuilingi 400.000 kutoka kwa Daud Njalu Silanga Mwenyekiti wa
UVCCM Mkoa wa Simiyu wakati alipochangia SACCOS ya Shina namba 15
shuleni Kata ya Migato.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji kwa
kikombe cha kiasili cha kabila la kisukuma mara baada ya kusimikwa chifu
Machibora Kinana.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana mwenye mgolole
mweusi akijumuika pamoja na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na
Uenezi kulia wakishiriki kula chakula cha asili ya kisukuma kinachoitwa
Michembe, kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk. Titus Kamani.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akihoji jambo kwa
Afisa Elimu Wilaya ya Itilima Ndugu Rogers Shimwelekwa wakati
alipotembeleaujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya ya Itilima jana,
kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Dk Leonard
Masale na wa pili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga lipu
pamoja na mafundi wakati alipotembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya
wilaya ya Itilima jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika eneo la Halmashauri hiyo.
Ndugu Nape Nnauye akipanda mti katika eneo la halmashauri ya Itilima.
Mkutano wa ndani ukiendelea chini ya mti.
Ndugu Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili ambayo ndiyo makao makuu ya Wilaya ya Itilima.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo jana.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakihutubia mkutano
wa hadhara katika kijiji cha Gangabilili makao makuuu ya wilaya ya
Itilima mkoani Simiyu.