MWANAMKE
mmoja anayefahamika kwa jina la Taraji Muenzi, 31, mkazi wa kijiji cha
Mwatasi, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, anashikiliwa na jeshi la
Polisi mkoani humo kwa kosa la kuichoma nyumba ya jirani yake na
kuwateketeza watoto wawili waliokuwa ndani mwake pamoja na vitu vyote
katika nyumba hiyo kwa kilichoelezwa wivu wa mapenzi.
Habari kutoka mkoani humo zinasema watoto walioteketezwa wakiwa ndani ya
nyuma hiyo ni Faraji, 6 na Jacob, 3 ambao walikuwa watoto pekee wa
Subira Kisitu aliyekuwa akituhumiwa na mtuhumiwa huyo kuwa anatembea na
mumewe.
Inaelezwa kuwa Taraji kwa muda mrefu alikuwa akimtuhumu jirani yake
kumuibia mume na kumchimba mkwara kwamba atamfanyizia, kiasi cha uongozi
wa eneo lao kuitisha kikao na kumtwanga faini ya Sh 10,000 aliotakiwa
kuilipa juzi, Juni 22 siku aliyofanya tukio hilo.Inaelezwa uongozi wa
kitongoji hicho kiliamua kumtoza faini baada ya wiki iliyopita kumvamia
jirani yake nyumbani kwake na kumwagia mboga na kusisitiza kuwa kuna
kitu atakachomfanyia ambacho hatasahau maishani kama siyo kwa kumuua kwa
sumu basi kwa kumchomea moto nyumba yake.
Hata hivyo inaelezwa kuwa jana juzi usiku akiamini kuwa jirani yake yupo
ndani na wanawe aliamua kuichoma moto nyumba hiyo, ila kwa bahati
mbaya jirani zake alikuwa klabuni akipata kinywaji na hivyo watoto
pekee waliokuwa wamelala ndani ndiyo waliougua na kufa pamoja na mali
zote.
Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza wanamshikilia mwanamke huyo ili kumfikisha
mahakamani kwa kitendo alichokmifanya ambacho kimeacha gumzo kijiji cha
Mwatasi, huku familia ya watoto ikiwa katika majonzi makubwa ya
kupoteza watoto wao.