NI
hakika ‘mtaa wa ngono’ umefumuliwa! Sakata hilo lilijiri saa tisa
usiku, Ijumaa iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Bamaga hadi
Sinza Mori jijini Dar eneo ambalo makahaba wameligeuza chumbani,
Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwepo ikifanya kazi chini ya uratibu
wa Ijumaa Wikienda. KWA NINI MTAA UFUMULIWE?
Kwa mujibu wa takwimu za kiserikali, eneo hilo
(kuanzia
Bamaga hadi Sinza Mori) limekubuhu kwa wasichana kujiuza nyakati za
usiku huku makao yao makuu yakiwa eneo la Afrika Sana hasa pembezoni mwa
Corner Bar.
Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa ya eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema:
“Tumejitahidi sana
kushirikiana na polisi ili kutokomeza ukahaba eneo hilo lakini wapi!
Hawa mabinti ni wabishi, mbaya zaidi wamelifanya eneo hili kuwa la
ngono.
“Watoto wetu wanapita usiku pale wanawaona wanavyofanya,
wanatuharibia kizazi kijacho, kama wao wamejishindwa wasiwaambukize
wengine.”
TIMU ILIYOENDESHA OPERESHENI
Siku
ya tukio, saa tisa usiku, askari wa ulinzi shirikishi walijipanga kwa
ajili ya kuufumua mtaa huo huku wakiwa na tahadhari kufuatia habari za
kiintelijensia kudai kuwa, makahaba hao walipanga kuua mtu punde
watakapovamiwa.
Askari hao wakiwa kwenye doria ya kila usiku,
waliwavamia makahaba hao eneo lenye majani madogo katikati ya Afrika
Sana na Mapambano upande wa yadi ya Mwanamboka wakiwa na wateja wao
wakifanya ngono hadharani.
NUSURA DAMU IMWAGIKE
Katika
hali iliyoonesha makahaba wamejiimarisha kwa ulinzi siku hizi, wakati
wa zoezi hilo, machangu hao sanjari na vibaka wanaowaunga mkono
wakisemekana ni ‘walinzi’ wao, waliokota mawe na kuwarushia askari hao
hali iliyozua tafrani zaidi.
Ndipo piga nikupige ilipozuka ambapo
askari walionesha umahiri wao wa kupambana na wahalifu kwa kuwadhibiti
kwa vichapo vya hapa na pale na kufanikiwa kuwaweka wengi chini ya
ulinzi.
Kuona hivyo, baadhi ya makahaba na wateja wao walifanikiwa
kuwachoropoka askari bila nguo na kutokomea gizani hivyo kulifanya eneo
hilo kuwa jeupe.

MAKAHABA WALIONASWA WALONGALicha
ya kuwa chini ya ulinzi mkali, baadhi ya makahaba walionaswa walikuwa
wakiwalalamikia askari hao kwamba wanawafuatafuata wakati kila mtu siku
hizi anaangalia atakulaje!
“Mnatuonea bure, nyie mnakula kivyenu na
sisi mngetuacha tule kivyetu, hao watoto wenu mnaosema tunawaharibu
usiku huu wao wanatokea wapi na wanakwenda wapi?” alisikika akisema
kahaba mmoja aliyekuwa mtata kuwekwa chini ya ulinzi.
Mwingine
akadakia: Kama mnataka tuwape uroda si mseme, mnatukamata kila siku
kwani tunawatibulia nini majumbani mwenu? Lini tumekuja kuwaghasi wakati
mmelala na wake zenu?”
Uchunguzi wa kawaida ulibaini kuwa muda rasmi
wa makahaba hao kuwasili eneo la Corner Bar ili kuanza ‘kazi’ ni saa
mbili usiku japokuwa wapo wanaoripoti mapema na kufanya biashara hiyo
kwa wizi kulingana na wateja wenye ‘kiu’ nyakati hizo.