TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM
Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1
Contacts Phone +44 74 04 863333, E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org
SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA JANGA LA BOMU JIJINI ARUSHA - TOKA CCM UK.
Chama
cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali
tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chadema uliofanyika
jijini Arusha hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu watatu na zaidi
ya watu 40 kujeruhiwa.
Tunatoa
pole zetu za dhati kwa familia za wafiwa na kwa wale wote waliojeruhiwa
katika janga hili la kikatili na kuwatakia uponaji wa haraka.
Tukio
hili limefuata badala ya lile la awali lililotokea katika kanisa
katoliki la mtakatifu Joseph mnamo tarehe 5 mei mwaka huu jijini Arusha,
ambapo pia lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya watu
60.
Ni
imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika
haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.
Tanzania
ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya
aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na
vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji
wa amani.
Tunawasihi
Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi
zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana
pasipo sababu. Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na
manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa
majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya
uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi
au umaarufu wa kisiasa .
Tunawasihi
WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi
wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.
Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi CCM UINGEREZA – UK.