Friday, June 21, 2013

BREAKING NEWSSSSS MEYA AFYATULIWA RISASI

Meya wa mji mkuu wa Uganda,Kampala amesema amepigwa na polisi waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake akizungumza na mwandishi wa habari akiwa kitandani Hospitalini meya huyo Erias Lukwago anasema alizilai baada ya gesi ya kutoa machozi ilipo tupwa ndani ya gari lake. Anaeleza kwamba maafisa wa polisi anasema walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake waki mshutumu kwa kuchochea ghasia.Meya huyo ni mpenzani wa rais wa nchini humu Yoweri Museveni. Mtu mmoja anaripotiwa kufariki na wengine kadha kukamatwa wakati wa ghasia hizo.Hatahivyo polisi wamekanusha madai ya kumpiga meya huyo ambaye pia ni mkosaji mkubwa wa rais Museveni. Upinzani unasema kuwa serikali inajaribu kukandamiza kilio cha mageuzi nchini humo.Katika tukio jingine kiongozi wa upinzani Kizza Besigy alikamatwa kwa kuandaa mkutano ambao polisi hawa kuidhinisha. Bwana Lukwago jana alikuwa anaelekea kwenye jopo maalumu kwa mara ya kwanza ambayo huenda ikamuondolea wadhifa wake kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.Mwandishi wa Habari Catherina Byaruhanga akiwa mjini Kampala ana sema kuwa,Polisi walizingila nyumba yake na kisha kumpeleka ambako jopo lilikuwa lina endesha vikao vyake. Lakini akiwa anapelekwa polisi walirusha vikebe vya gesi ya kutoa machozi ndani ya gari lake.Walinipiga kifuani na kudai na chochea ghasia walinirarulia nguo zangu na kunitesa kwa kila njia nilijaribu kuwambia wani ache lakini sikufanikiwa alisema Lukwago. Kizza Besigye amedaiwa na polisi kuchochea umati wa watu mjini Kampala ili kumuunga mkona bwa Lukwago kosa ambalo ofisi yake imekanusha.