BREAKIN NUZZZZ Ccm wapata ajali pemba
Makada 14 wa CCM wajeruhiwa ajalini
Na Hamad Shapandu, Pemba
MAKADA 14 wa CCM wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kutoka Micheweni kwenda Konde kisiwani Pemba,kupoteza
mwelekeo na kugonga mti.
Gari
hilo aina ya Minibus yenye namba za usajili Z505 BQ iliyokuwa
ikiendeshwa na Humud Seif Humud ilipata hitilafu hiyo muda mfupi baada
ya kuondoka kituo cha magari Micheweni ikiwa imebeba wajumbe wa Kamati
ya Siasa ya CCM, wilaya ya Micheweni.
Mganga wa hospitali ya
Micheweni, Dk. Amour Suleiman Khamis alisema majeruhi wote 14
walifikishwa katika hospitali hio na baadhi yao walikuwa wameumia
vibaya.
Alisema abiria 10 walitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani, huku wengine wakiendelea na matibabu.
Aliwataja walioumia kuwa ni Salimu Busaga Dida mkaazi wa Makangale,
Halima Abeid wa Msuka, Omar Hamad Sheha, Khamis Juma Faki wa Konde,
Msellem Kombo, Abdi Said na Amina Khatib Ali wa Msuka.
Wengine
ni Riami Khamis Shaame, Ramadhan Omar Ahmed, Hadia Khamis Juma wote
wakaazi wa Konde, Juma Omar Khamis wa Kifundi, Muhammad Ali wa Kicha,
Kidawa Suleiman Khatib na dereva wa gari hilo, Humud Seif.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi na Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis walikuwa
miongoni mwa viongozi waliokwenda kuwafariji majeruhi hao na kuwataka
wawe na subira katika wakati huu mgumu.
Majeruhi Riami Khamis
Shaame na Ramadhan Omar Ahmed walisema gari hilo halikuwa na mwendo wa
kasi bali hitilafu za kufunguka ‘tairod’ ndio chanzo cha ajali hiyo.
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa hususan viongozi wa CCM,
wafanyakazi na wananchi wanaendelea kuwajulia hali katika hospitali
waliyolazwa.