Habari
zilizoifikia muda huu kutoka Dodoma zinaripoti kwamba
Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses
Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la,
tukio hilo limetokea jioni hii wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake
mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana
kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni
naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera
vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya
Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na
kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi
kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo
kikali kilipoanzia.
Shuhuda
wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli
amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye
kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Kua nasi tutazidi kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tukio hili kadiri habari zitakavyozidi kupatikana.