Serikali
ya jimbo la Lagos Nigeria, imesema sehemu ya jengo lililoaanguka katika
kanisa la Synagogue Church of All Nations, ambalo lilijengwa kwa ajili
ya kufikia wageni lilijengwa bila kibali cha Serikali.
Kamishna anayesimamia mipango miji
Lagos, Olutoyin Ayinde amesema uchunguzi uliofanywa na tume iliyoongozwa
na Oyetade Komolafe umeonyesha hakuna kibali kilichotolewa na mamlaka
hiyo kuidhinisha ujenzi wa jengo la ghorofa sita.
Amesema kibali kilichotolewa kilikuwa
cha ujenzi wa jengo la kanisa ambalo ni ukubwa wa ghorofa tano pekee, na
uchunguzi umebaini kibali hicho kilikiukwa kwa kujengwa ghorofa nane
badala ya tano.
Anyinde amesema mamlaka hiyo imeagiza
mamlaka ya anga kuchunguza juu ya ndege ambayo imedaiwa kuzunguka jengo
hilo muda mfupi kabla ya jengo kuanguka.
