
Mechi
ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana Machi 30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam
imeingiza jumla ya sh. 26,455,000,amabyo ilikua na Watazamaji 4,741
walikata tiketi kushuhudia pambano hilo ambapo Azam iliibuka na ushindi
wa mabao 2-1.

Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000,mgawanyo kwa mapato
ulikuwa kama ifuatavyo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
4,035,508.47,gharama za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu
ilipata sh. 5,460,687.63,uwanja sh. 2,776,620.83,gharama za mechi sh.
1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh. 1,665,972.50.
Mapato mengine yalienda kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu
(FDF) sh. 832,986.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 647,878.19.