![]() |
Mgeni rasmi Bi. Sophia Simba (Mwenyekiti UWT Taifa) akimkabidhi Kadi ya UWT mmoja ya wanachama wapya Mwanafunzi msomi wa Vyuo Vikuu Jijini Mwanza Malimbe Nyegezi. |
![]() |
Zoezi la kuwakabidhi Kadi wanachama wapya likiendelea. |
![]() |
Sehemu ya Umati wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali waliohudhulia Kongamano hilo. |
![]() |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu akiwa na Viongozi na Makada wa CCM wakati wa Kongamano hilo. |
![]() |
Lucy Mlula na Editha Paul wakisoma risala ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanachama wa UWT Jijini Mwanza wakati wa Kongamano hilo. |
![]() | ||
Wakati wa kupata picha za kumbukumbu na mgeni rasmi. |
Na PETER FABIAN.
MWANZA.
VIJANA wasomi wa Vyuo
Vikuu Mkoani Mwanza wanachama wa CCM na Jumuiya ya Wanawake (UWT)
wamesema kwamba bado tatizo la Ajira ni kikwanzo kikubwa kwa wanavyuo
wahitimu na wanaoendelea vyuoni kujiunga na Chama cha Mapinduzi na
Jumuiya zake.
Kauli hiyo ilitolewa
jana na wanachama wa CCM na UWT wasomi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vingine
vilivyopo Jijini Mwanza wakati wa risala yao kwa mgeni rasmi wa
Kongamano kubwa la kujadili Maendeleo ya Mwanamke ndani ya miaka 52 ya
Uhuru mbele ya Mwenyekiti wa UWT Sophia
Simba (Mjumbe wa NEC CCM Taifa) na Waziri wa Wizara ya Wanawake Jinsia
na Watoto katika ukumbi wa Masista wa Kanisa Katoliki Malimbe Nyegezi
Jijini hapa.
Wakisoma risala hiyo
iliyoandaliwa na wanavyuo vikuu na vingine Mkoani humo walieleza kuwa
pamoja baadhi yao kuhitimu na wengine kuendelea na masomo bado hali hii
ya ukosefu wa ajira hukatisha tamaa kwa wahitimu na wanavyuo
wanaoendelea katika kujiunga na CCM na Jumuiya zake jambo ambalo Chama na Serikali yake inapaswa kuliangalia kwa upana zaidi na kuliwekea mikakati ya kulipunguza ukubwa wake.
Wasomi hao pia walieleza kuwa lengo la kongamano hili ni kupata uelewa juu ya
Maendeleo ya Mwanamke ndani ya miaka 52 ya uhuru na kufahamu kwa undani
juu ya Historia ya UWT kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kujitathimini kwa
wasomi wanawake walioko vyuo vikuu na waliohitimu.
Lucy Mlula na Edita Paul
wakisoma risala hiyo walieleza kuwa Hali ya kisiasa katika vyuo vikuu
na vingine ni nzuri kwa wastani ikilinganishwa na kipindi cha miaka
mitatu iliyopita hii ni kutokana na kuimarisha Wanachama wa CCM na
Jumuiya za UWT na UVCCM katika vyuo hivi ikiwa ni kuongeza idadi ya
wanachama wapya na kuendelea kueneza sera za CCM kwa wanavyuo wenzetu na
jamii inayozunguka vyuo hivyo.
“Sisi wanafunzi Vyuo Vikuu Mkoani Mwanza ambao pia ni wanachama tunayo
mikakati mbalimbali ya kuimarisha Chama na Jumuiya na kufanya Midahalo
mbalimbali itakayowahusisha wanachama na wasio wanachama kwa lengo la
kujifunza na kujua Itikadi, Sera, Ilani na Malengo ya Chama ikiwa ni
nguzo mhimu ya kukiimarisha Chama cha Mapinduzi” walieleza katika risala
yao.
Wanafunzi wa Vyuo vikuu vyote Mkoani Mwanza hawakusita kumpongeza Mjumbe
wa NEC CCM Taifa kutoka Wilaya ya Tarime Christopher Gachuma kama
mfadhili mkuu wa Kongamano hilo wafadhili wengine kwa mchango yao ya
fedha na ushauri mzuri iliyopelekea kufanikisha shughuli hiyo.
Naye Waziri Simba akizngumza na wanavyuo vikuu na vingine Mkoani humo
walio wanachama wa CCM na Jumuiya ya UWT aliwapongeza kwa kutenga muda
wao na kuandaa na kushiriki kongamano hilo kwa wanachama wa UWT na CCM
jambo ambalo litaongeza chachu kwa wasomi waliopo vyuo vikuu na wahitimu
kujiunga na CCM na Jumuiya zake.
“Kwanza niwahase vijana wasomi ambao ni wanawake kwanza mjitambue, pili
msome kwa bidii na tatu acheneni na mambo ya wanaume kwani wanaume
‘Noma’ mnapendeza leo kutokana na kuwa wasomi na wanaume watawapenda
mkiwa wasomi tu na mwanaume hawawezi kukupendezesha ukiwa si msomi
hivyo ni vyema mkajitambua sasa na m kuwa wakakamavu na wapambanaji
zaidi” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo wa Taifa wa UWT aliwaeleza wasomi hao wanawake wanachama
wa jumuiya hiyo kuwa zamani mtoto wa kike hakupewa msukumo wa kupata
elimu ya juu kwa baadhi ya makabila na wengi wao ilikuwa ni vigumu
kufika darasa la nne wakati huo lakini sasa CCM naSerikali yake ikaweka
mikakati na kujenga shule za msingi kila Kijiji, Sekondari za Kata, Vyuo
vya Ualimu, VETA na Vyuo Vikuu vya serikali na binafsi.
“Mwanza zamani ilikuwa na sekondari tatu tu ambazo niza serikali ambazo
ni Ngaza, Bwiru Girls na Boys lakini leo shule lukuki na zamani nchi
zima Vyuo vikuu vilikuwa vitatu tu ambavyo ni Chuo Kikuu Mlimani na
Mhimbili (Dar es salaam) na Mzumbe (Morogoro) sasa viko kila kona ya
nchi hii vya serikali, mashirika ya dini na watu binafisi hivyo kazi ni
mojas tu kwa wanawake kusoma kwa bidii” alisema.
Waziri Simba alisema kuwa ni mwiko kwa mwanamke kukata tamaa ya kusoma
na kuchukua Shahada na Sitashahada eti kutokana na tatizo la ajira na
badala yake mjitahidi kuhitimu na kufanya vyema katika taaluma
mlizosomea na sasa anzeni kuweka mikakati na mipango ya kujiunga na
kuanzisha kikundi pindi mnapohitimu tayari mnakuwa na ajira na zaidi ni
kuomba serikalini msaada na serikali itawasaidia.
“Wasomi acheni kuchagua kazi jambo la kuchagua kazi ni lazima mtambue
kuwa ni kosa kubwa kuchagua kazi na tumieni taaluma zenu kuanzisha
vikundi vya kujiajiri na kuanzisha ajira kwani serikali bado inatambua
kuwepo tatizo la ajira lakini imekuwa ikiajiri kulingana na nafasi
zinazopatikana kwani si wasomi wote wataajiliwa.
Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma alisema
kwamba pamoja na mambo yaliyojitokeza lazima kuwe na Kanuni za kusaidia
kuliongoza kwani bila kuwa na Kanuni mambo hayatakwenda zaidi itakuwa ni
vurugu tupu kwa kutambua hilo kuundwa kamati za kushughulikia suala
hilo na sasa mjadala na hoja ni jinsi gani kuzipitishe katika kufanya
maamuzi ya Katiba hiyo kwa miaka hamsini ijayo.
“Lakini napenda kuwahakikishia kuwa wanawake wote bila kujali Itikadi
zetu za kisiasa tumeamua kuungana wa vyama vyote vya kisiasa, mashirika ,
NGOs, Taasisi na Mawaziri na Wabunge kuhakikisha tunatetea vyema hoja
ya asilimia 50% kwa 50 % ili mwanamke ashiriki katika uongozi na kutoa
maamuzi” alisisitiza.
Wito wangu kwenu wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu na vingine msikubali
kudanganywa na baadhi ya watu na wanasiasa kuwatumieni kuwaunga mkono
katika kulisambaratisha Taifa letu hili kwa uchu na tamaa za madaraka
kwani wengi wao ni wabinafisi na wenye lengo la kutawala kwa kusema
uongo na kuwataka ninyi muwaunge mkono ili wafikie malengo yao hivyo
kataaeni kutumika kwa hili.
Kongamano hilo lilihusisha wanavyuo zaid 600 kutoka matawi ya Vyuo Vikuu vya St. Agustine (SAUT)
Malimbe cha Nyegezi , Sokoine CBE, Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya na
Tiba Cha Katoliki(CUHAS) Bugando, Mipingo, VETA vya Ufundi ,
UALIMU Butimba, KILIMO cha Ukiriguru, MIFUGO Cha Mabuki, UVUVI cha
Nyegezi na vingine vyenye matawi yake Jijini Mwanza na vilivyopo Mkoani
Mwanza.