
Stori hii ina pande nyingi sana ambazo zitazungumza kupitia hapa hapa na hapa tupo na baba yake mzazi Dogo Janja ambaye anaelezea jinsi alivyoyapokea maamuzi ya Dogo Janja>>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake’
‘Akishafanya maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana kuwa nataka kufanya jambo hili au la,mimi tayari alishawahi kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.