
Unaweza kujaribu kufikiria uone jinsi hili jambo lilivyo zito.. ndege ya abiria imepotea kwa zaidi ya siku 11? sio kwamba imepata ajali.. yani imepotea na haijulikani ilipo kwa zaidi ya siku 11? msako umefanyika kwenye nchi zote ambazo labda ingekua huko kwa huo muda lakini hakija onekana kitu.
Taarifa iliyotoka kwa Wavuvi wawili waliohojiwa March 19 2014, inasema wawili hawa ambao wakati huo walikua baharini wamethibitisha kuiona ndege kubwa ya abiria ikipita chini sawa na urefu wa miti.

Ndugu wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege wameonekana kukata tamaa ya kusubiria ndugu zao sasa hivi, mama mmoja mwenye ndugu kwenye ndege hii, Jumatano ya March 19 2014 alibebwa baada ya kulilia ndugu yake kwa sauti kwenye mkutano na Waandishi wa habari.
Taarifa kuhusu hii ndege ni nyingi, ni siku moja tu imepita toka nisikie kwamba muda mfupi baada ya ndege kupaa kutokea Malaysia, kuna mtu alizima kifaa kinachohusika na mawasiliano na kuonyesha mwelekeo pamoja na speed ya ndege.
