
Baada
ya kupata taarifa za kuwepo kwa dhehebu hili ambalo linakataza watoto
kwenda shule na wagonjwa kutibiwa hospitalini, Serikali ilimkamata
kiongozi wake pamoja na waumini kadhaa lakini baadae wakaachiwa huru.
Alieanzisha hili dhebebu anaitwa MEDADI LAURENT ambae baada ya kukamatwa alihukumiwa kifungo cha miezi miwili jela au faini ya shilingi 30,000/.
Anasema ‘kama ni baridi unapaswa uwe baridi, kama ni moto
unapaswa uwe moto, kama nilivyosema toka mwanzo mimi mpaka dakika ya
kufa sina mpango wa kusomesha mtoto isipokua kile serikali itachoamua
ndio ifanye’
Mmoja wa waumini wa kike wa kanisa hili ameiambia millardayo.com
kwamba ‘sisi elimu tunayoijua ni elimu ya kumfahamu mtakatifu alie juu
maana ndipo kuna uzima lakini katika elimu ya dunia hakuna uzima, maana
tunawashuhudia wasomi wengi wakifa hawapati uzima lakini sisi hata
tusiposoma elimu ya dunia hii kama tutamtii Mungu au hata kama tutakufa
tutakua na uzima wa baadae’
Muumini mwingine wa kiume kaiambia millardayo.com
‘swala la elimu siafikiani nalo kwa sababu kwanza kwa mujibu wa
maandiko matakatifu hatupaswi kujifunza elimu nyingine tofauti na elimu
ya kumjua Mungu maana ukisoma Yohana anasema na uzima wa milele ndio huu
wakujue wewe Mungu wa pekee na Yesu kristo uliemtuma.
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Peter
Toyima amesema ‘tumeandika barua kuliandikia lile dhehebu kwamba ni
marufuku kuendelea na shughuli hizi kwa sababu kwanza hawajasajiliwa kwa
hiyo hamna uhalali wa kuwepo na wakifanya tena mkusanyiko wa namna hiyo
lazima tuwakamate na hatua zichukuliwe tena.
Dhehebu la Sabato Matengenezo lilianzishwa January 2014 baada ya kujitenga kutoka katika dhehebu la Waadventista wasabato.