
Zitto Kabwe
hicho, kusikiliza rufaa ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kama inavyodaiwa
na baadhi ya watu. Amesema chama hicho kitaitisha kikao hicho wakati wowote kuanzia sasa, ili kusikiliza
utetezi wa Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini. Akihutubia mamia ya wakazi wa Manispaa ya
Iringa na vitongoji vyake katika uwanja wa Mwembetogwa juzi, Dk Slaa alisema Zitto alivuliwa nafasi zake za uongozi ndani ya chama hicho baada ya kubainika amekiuka maadili ya chama. “Hata ikitokea mimi au Mwenyekiti wangu, Freeman Mbowe au kiongozi au mwanachama yeyote amevunja maadili ya chama, ni lazima atafukuzwa; huu ni utaratibu wa chama na ni lazima usimamiwe,” alisema.
Alisema hivi sasa Zitto haruhusiwi kufanya shughuli za kichama kupitia
jukwaa la Chadema kwa kuwa si kiongozi tena wa Chadema, rufaa yake
haijasikilizwa na kafungua kesi mahakamani. “Wanachama, wapenzi na wadau
wote wa Chadema msimpe ushirikiano wowote Zitto mpaka suala lake
litakapohitimishwa,” alisema.Alisema Operesheni ya M4C Pamoja
Daima, haifanywi na chama hicho kumshughulikia Zitto, inafanywa kama
maandalizi ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo, wakati Zitto kupitia gazeti moja la kila
siku, akikaririwa kutangaza kuanza mikutano ya kuzungumza
na Watanzania.
“Kama kuna mtu anadhani sitaweza kufanya mkutano wa aina yoyote katika
maeneo mbalimbali nchini anajidanganya, nitazunguka kuzungumza na
wananchi kwa maslahi ya Taifa
hili na ni haki yangu kikatiba,” alikaririwa Zitto
hili na ni haki yangu kikatiba,” alikaririwa Zitto