
Mawaziri wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya, wameamua kuwawekea vikwazo washukiwa wa ghasia zinazoendelea nchini Ukraine.
Waziri
wa Italia, Emma Bonino, amesema kuwa watu aliowataja kuwa na damu
mikononi mwao, watakabiliwa na vikwazo ikiwemo vikwazo vya usafiri,
pamoja na kupiga tanji mali zao.
Pia kutakuwa na marufuku ya kuingiza nchini humo vifaa vya polisi wa kupambana na ghasia.
Mawaziri
wengine wa mambo ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, kutoka Ufaransa,
Poland na Ujerumani, wako mjini Kiev kushauriana na pande hizo mbili.
Wanakutana na viongozi wa upinzani baada ya mkutano wao na Rais Viktor Yanukovych kuhusu mwafaka wa amani.
Hii bila shaka itajumuisha swala la kuunda serikali ya mpito.
Watu
22 wameuawa katika ghasia zilizozuka upya kati ya waandamanaji na
polisi mjini Kiev Ukraine, baada ya makubaliano yaliyofikiwa kutibuka.
Watu
nchini humo wameelezea kujionea mabomu ya petroli , risasi na maji
vikitumiwa katika kitovu cha maandamano, medani ya uhuru.
Walioshuhudia ghasia hizo wanasema kuwa karibu watu 21 na 27 wameuawa.
Polisi mmoja ameripotiwa kuuawa.