
Mashabiki wa Timu ya Simba, walimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini jana machana.
Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar.

Kumekuwa
kukitokea furaha kwa mashabiki, viongozi na hata wachezaji wa Klabu
zetu kubwa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha au
Mchezaji mpya kwa kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea
kakosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu
husika,anaweza kutimuliwa ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya
kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.

Kocha mpya wa Simba SC, Mserbia Zdravko Lugarusic amesaini Mkataba wa
miezi sita mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC,
Zacharia Hans Poppe leo mchana Mbezi, Dar es Salaam.