
Gavana wa Hawaii amesain mswada wa kuruhusu ndoa za jinsia moja baada ya watu wanaokata ndoa za jinsiia kuomba kuhalalishwa kwa ndoa hizi, ombi ambalo walilitoa zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Ndoa zinaanza kufungwa tarehe mbili December ambapo Hawaii litakua jimbo la 15 la Marekani kuhalalisha ndoa za jinsia moja.
Gavana huyu ambae anaunga mkono ndoa za jinsia moja amesema alifarijika kusikia kutoka kwa rafiki yake ambae ni msagaji akisema kwamba siku hii ya kusain huu muswada, ni siku kubwa sana kwa jamii ya wanaozitaka ndoa za jinsia moja kwa sababu wameisubiria hii kwa miaka mingi sana.

Sio kwamba kuna majimbo 14 yamepitisha ndoa za jinsia moja ndio ikufanye uona Wamarekani wanakubali ndoa hizi, kuna watu wanapinga kabisa yani na wanaandamana wakisema hii ni dhambi kubwa ya kiama, toka hii ishu imeanza Hawaii kuna watu waliandamana na magari yao kwa kupiga honi wakipinga kabisa.
Kitu ambacho sio kawaida ni kwamba kwenye upitishaji wa muswada huo huko Hawaii, Wananchi waliruhusiwa kuongea ambapo zaidi ya watu elfu moja walipinga ndoa hizi za jinsia moja ndani ya siku tano zilizotolewa kwa ajili ya kila mmoja kutoa maoni.