
Yani sasa hivi Wanamuziki wa kimataifa kujichanganya na Wanamuziki wa Afrika kwa siku za karibuni sio tena habari ya kushtua…. zamani kidogo haikuwa kawaida ila P Square walipokolabo na Rick Ross, D’Banj na Kanye West, Ay na Sean Kingston pia na Romeo kidogo ikaanza kuonekana hakuna kinachoshindikana.
Hizi picha ni za Akon akiwa na Wanigeria Wizkid na Banky W somewhere in Ghana ambako wanafanya shooting ya music video ya hit single ‘Roll it’ ambayo itaanza kuonekana baada ya siku kadhaa.
Wizkid anakwambia katika vitu ambavyo hakuwahi kuvitarajia ni kuingia kwenye line na mastaa wakubwa wa dunia kama vile Wale, Rick Ross, Busta, Akon na Chris Brown ambae aliwahi kumtaja mpaka kwenye interview na kumsifia kwamba Wizkid ni talent kali kutoka Afrika.
