
Viongozi hao walikutana leo wakati wa mkutano wa faragha katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. (HM)
Aidha vingozi wa kamati sita wakiwemo, mawaziri kutoka nchi hizo mbili pia walikutana wakati wa mkutano hio na kujadili maswala kuhusu nchi hizo mbili.
Rais wa Sudan
Kusini Salva Kiir Mayardit alielezea furaha yake kwa kufikia makubaliano
ya pande hizo mbili akisema kuwa serikali yake itajitolea kuhakikisha
kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa.
Kwa upande
wake Rais Umar al-Bashir alisema kuwa mkutano ulifanikiwa na kuongeza
kuwa serikali yake itajitolea kuhakikisha kuwa makubaliano waliyoafikia
yanatekelezwa.
Marais hao
walifanya mkutano wa faragha muda mfupi baada ya Bashir kuwasili na
wajumbe wake wa Sudan katika Ikulu ya Rais mjini Juba.
Kwa mujibu wa
shirika la habari la SUNA, baadhi ya maswala yaliyojadiliwa kwenye
mkutano huo ni mambo tete kuhusu Abyei,usalama pamoja na kutekelezwa kwa
makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Mnamo siku ya
Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial
Benjamin, aliambia kituo cha redio cha Sudan CRN kuwa marais hao wawili
watazungumzia mgogoro wa Abyei katika kutaka kuboresha uhusiano kati ya
nchi hizo mbili.
Kuhusu swala
la kura ya maoni kuhusu Abyei , waziri alisema kuwa Muungano wa Afrika
hauruhusu uamuzi wa pande moja kuhusu kura ya maoni.
Aliongeza kuwa Kura ya maoni lazima iruhusiwe na nchi hizo mbili na kuidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Aidha alisema
kuwa sudan Kusini inashurutishwa na makubaliano ya ushirikiano kati ya
nchi hizo mbili na kwa hivyo haiwezi kuunga mkono kura ya maoni
inayoshinikizwa na upande mmoja.
Hata hivyo
alisema anaelewa kwa nini jamii ya Abyei iliamua kupiga kura ya maoni
kujitenga na ni kwa sababu ya masaibu waliyoyapitia.
Alisisitiza
kuwa Muungano wa Afrika na Sudan lazima ziisikilize jamii ya Abyei na
kukubaliana kuhusu tarehe ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kutaka
kujitawala wenyewe. Chanzo: bbcswahili