Katika
hali tofauti waliyokutana nayo wanunuzi wa bidhaa kutoka kwenye maduka
mbalimbali yaliyopo kwenye mall ya Mlimani city, wengi wameona ni hatua
nzuri baada ya kuongeza usalama wa watu wanaotumia jengo hilo hasa
kutokana na mambo yaliyotokea huko Kenya. Tofauti na jana, leo hii
jumapili 6/10, wateja wote waliokuwa wanaingia kwenye mall hiyo walikuwa
wanasachiwa na mashine maalum pamoja na mabegi yao.
Mdau wetu
alifika kwenye mall hiyo kwa manunuzi ya kawaida na alikuta askari
wanaohusika na ulizi wakiwa wametengenisha njia mbili, moja ya kutoka na
nyingine ya kuingia kwenye kila mlango wa kuigia kwenye mall. Askari
wawili mmoja wa kike kwa ajili ya wateja wa kike na mwingine wa kiume
pamoja na askari wa tatu kwa ajili ya kusachi mabegi. Baadhi ya watu
walionekana kufurahia hatua hiyo ambapo siku kadhaa zilizopita, watu
wengi walianza kujiuliza maswali juu ya usalama hasa wakifi wa watu
wanaongia kwenye mall hiyo kwa ajili ya manunuzi yao ya kila siku. |