Tuesday, October 15, 2013

SIKU CHACHE KABLA YA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA YAIBUA VIHOJA,NGASA AHAIDI KUCHOMA NYUMBA ZAKE KAMA HATA IFUNGA SIMBA

 

 

 

MRISHO NGASSA "NITACHOMA MOTO NYUMBA ZANGU TANO KAMA SITAIFUNGA SIMBA JUMAPILI"

Saleh "Jembe" anamkariri mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa akisema kuwa hasira zake ni kama atashindwa kufunga au angalau kutoa pasi itakayozaa bao litakaloimaliza Simba: “Niko vizuri na ninajiona niko tayari kwa mchezaji, nataka kufanya kazi nzuri na ninajua Simba nitawafunga.  Kama nitashindwa kufunga basi nitatoa angalau pasi ya bao litakalosababisha Simba wafungwe. La sivyo nitachoma nyumba zangu tano ninazomiliki,” alisema Ngassa kwa kujiamini.

Yanga na Simba zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.