Wednesday, October 30, 2013

MTANZANIA AIWAKILISHA AFRICA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA UFUNDII





Watalaamu wa ICT kutoka nchi mbali mbali duniani wakiwa kwenye kikao cha kamati ya ufundi ya International Association of Ports & harbours(IAPH) inayoshugulikia Trade Facilitation & Port Community system, kuuliza ni Ndg. Magesa anaewakilisha bara la Afrika katika Kamati hiyo




Wajumbe wa mkutano huo walipata maelezo kutoka Mhandisi wa mifumo ya mawasiliano wa Bandari ya Sines, Ureno


Wajumbe wa mkutano walipata nafasi ya kutembelea chumba cha mawasiliano cha Bandari ya Sines, Ureno



Hapa ni katika chumba cha dawati la Msaada wa mifumo yote ya mawasiliano na Teknolojia katika Bandari ya Sines, bandari hii ndio bandari kubwa Portugal na mifumo yake yote ya ICT imeunganika na ya wadau wote ikiwa ni pamoja na idara Forodha na wadau wengine




Hapo ni ndani ya Control Tower ya Bandari ya Sines, Portugal

Kamati ya ufundi ya IAPH ni kamati muhimu na ina jukumu kubwa la kuhakikisha Bandari zote ulimwenguni zinakuwa na mifumo bora na ya kisasa ya mawasiliano kutumia Teknolojia ya habari (TEHAMA ) na mifumo hii iweze kuwasiliana na wadau wote wa biashara ya kibandari na Forodha ndani ya nchi husika, na nje ya nchi na mabara yote. Bado nchi nyingi za kiafrika ziko nyuma katika matumizi ya mifumo hii na mwaka huu ndio bara la Africa lilipata mwakilishi katika Kamati hii Ndg. Magesa(Mkuu wa idara ya ICT-TPA) ambaye alichaguliwa katika mkutano Mkuu wa Bandari zote ulimwenguni uliofanyika Los Angeles, USA, May 2013. Tanzania iko katika hatua muhimu za utekelezaji wa mradi wa Electronic Single Window System na miezi michache ijayo itaanza matumizi ya mfumo huo.