Michuano
ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champions league
imeendelea usiku wa jana kwa michezo nane ikiwa ni sehemu ya kwanza ya
raundi ya pili ya hatua ya makundi .
Klabu ya Arsenal iliendeleza mwanzo wake mzuri baada ya kuifunga Napoli kwa mabao mawili bila .
Arsenal ambao wako kundi F walifunga mabao yao kupitia kwa Mesut Ozil huku Olivier Giroud akifunga bao lingine .
Katika
mchezo mwingine wa Kundi F Borrusia Dortmund waliwafunga Olympique
Marseile kwa matokeo ya 3-0 . Marco Reus na Robert Lewandowski ndio
waliofunga mabao ya Dortmund ambapo Lewandowski alifunga mabao mawili .
Matokeo
hayo yanamaanisha kuwa Arsenal wanaongoza kundi hilo wakiwa wamekusanya
pointi sita baada ya mechi mbili huku Napoli na Dortmund ambao
wameshinda na kupoteza mechi moja moja wakiwa na pointi tatu na Marseile
hawana pointi yoyote .
Katika
michezo mingine Fc Barcelona waliwafunga Glasgow Celtic 1-0 bao pekee
la mchezo huo likifungwa na Cesc Fabregas . Kwingineko Ajax Amsterdam na
Ac Milan walitoka sare ya 1-1.
Fc
Porto wakiwa nyumbani kwao walipoteza mchezo wao dhidi ya Atletico
Madrid kwa matokeo ya 2-1 . Porto walianza kufunga kupitia kwa Jackson
Martinez lakini Madrid walisawazisha kupitia kwa Arda Turan na Diego
alifunga bao la ushindi .Mchezo mwingine wa kundi hilo hilo ulishuhudia
Zenith St Petersburg na Austria Vienna wakitoka sare ya 1-1.
Huku
jijini Bucharest Chelsea hawakuwa na Huruma mbele ya wenyeji wao Steau
Bucuresti baada ya kuwafunga 0-4 . Wafungaji wa Chelsea katika mchezo
huo walikuwa Ramires aliyefunga mabao mawili , Frank Lampard huku Mlinzi
wa Bucuresti Daniel Georgievski akijifunga mwenyewe kwenye bao lingine .
Schalke 04 wakiwa ugenini nchini Uswisi waliwafunga Fc Basel 1-0 . Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Jullian Draxler .
Michuano
hiyo itaendelea hii leo ambapo Manchester United watakuwa wageni wa
Shakhtar Donetsk huko Ukraine , Real Sociedad watasafiri hadi nchini
Ujerumani kucheza na Bayer Leverkusen , Real Madrid watawakaribisha Fc
Copenhagen huku Juventus nao wakiwa wenyeji wa Galatasaray .
Michezo
mingine itawashuhudia Manchester City wakicheza na mabingwa watetezi
Bayern Munich , Viktoria Plzen nao wakicheza na CSKA Moscow pamoja na
Paris St Germain dhidi ya Benfica na Anderletch wakicheza na Olympiakos.