Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana
na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa
vya michezo muda mfupi kabla ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo
vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es
salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea
vifaa vya michezo kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Kelvin Twissa. Vifaa hivyo vitatumika kwenye mashindano maalum ya
Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim. Vodacom ilikabidhi jezi za soka seti 12, mipira 40
na kombe kubwa la Mshindi

Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea
kombe kubwa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin
Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa mashindano maalum kwa shule
za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.Kushoto ni
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi pia
jezi za soka seti 12 na mipira 40.

Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala akiongea na
waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali vya
michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa ajili ya mashindano maalum kwa
shule za sekondari za mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.

Waandishi wa
Habari wakimfuatilia Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.
Fenela Mukangala wakati akiongea kwenye hafla ya kupokea vifaa
mbalimbali vya michezo kutoka Vodacom vitakavyotumika kwenye mashindano
maalum ya shule za Sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na
Wizara.

Mkuu wa Masoko
na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa akifanunua jambo kwa Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala wakati
walipofanya mazungumzo mafupi baada ya hafla ya amkabidhiano ya vifaa
vya michezo kwa ajili ya mashindano maalum ya shule za Sekondari za Mkoa
wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum
Mwalim.
Vodacom yakabidhi vifaa kwa Waziri Mukangala vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala leo amepokea
vifaa vya michezo kutoka Vodacom kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano
maalum ya sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es
salaam.
Akipokea vifaa
hivyo ambavyo ni jezi seti 12 na mipira 40 pamoja na kombe kwa ajili ya
bingwa wa michuano hiyo Waziri Dk Mukangala ameelezea kufurahishwa
kwake jinsi ambavyo Vodacom walivyopokea ombi la Wizara la kusaidia
mashindano hayo.
Amesema lengo
la mashindano hayo ni kuendeleza azima ya serikali ya kutengeneza fursa
ya ukuzaji na uendelezaji michezo kwa ngazi za chini kupitia falsafa ya
michezo jamii.
"Michezo ni
gharama inahitaji fedha nyingi kugharamia vifaa, mafunzo kwa walimu,
viwanja na gharama nyengine za uendeshaji ndio maana naipongeza sana
Vodacom kwa kukubali ombi letu la kusaidia mashindano haya maalum
yatakoyoshirikisha shule 12 za sekondari za Mkoa wa Dar es
salaam."Alisema
"Mashindano
haya ni ya majaribio tukiangalia namna ambavyo tunaweza kuwekeza vya
kutosha kwenye michezo ngazi ya mashuleni kwa nchi nzima, tutaanza na
mchezo wa soka ila mipango ni kupanua wigo kwa kuongeza mpira wa pete na
riadha kwa hapo mwakani ikihusiha mikoa mingi zaidi."Alisema Dk.
Mukangala
Waziri Dk.
Mukangala amesema Wizara yake inaimani kubwa juu ya mpango huo huku
akizitaka jamii kuyapokea na kuyaona kuwa ni sehemu yao ili pamoja na
kuyapapa mafanikio bali pia kuwatia moyo watoto wakati wote watakapokuwa
waskishiriki.
Amesema kuwa
anatambua kuwa mahitaji ni makubwa na kwamba kila shule hapa nchini
ingependa kushiriki lakini kwa kuanzia watachagua shule 12 za sekondari
kama majaribio huku mipango ikiendelea kuwekwa sawa ili mashindano hayo
yawe mapana zaidi kwa hapo mwakani.
"Tuna shule
nyingi hapa tu Dar es salaam tumepata wakati mgumu sana kuchagua
wawakilishi wa kila Wilaya lakini kwa sasa tunaanza na hizo chache
tukiwa na Vodacom na baada ya kumalizika tutafanya tathmini kuona namna
ya kuyaongezea wigo wa ushiriki na wa kijiografia."Alisema Dk. Mukangala
Kwa upande
wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa
amesema Vodacom inatambua umuhimu wa kuwaandaa wachezaji katika ngazi za
chini ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya michezo nchini.
"Kukubali
kwetu kuwa wadhamini kumesukumwa na imani yetu juu ya maendeleo ya
michezo nchini tukiamini katika kuwekeza kwa wanafunzi mashuleni, leo
tunafuraha kuwa sehemu ya miapngo ya serikali kukamilisha kile ambacho
kila mtu anapenda kukiona kikifanyika katika michezo."Alisema Twissa
"Tumekuwa
wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa
kimaendeleo hasa kwenye eneo la ushindani hivyo ili mafanikio hayo yawe
endelevu ni lazima tuwe na misngi mzuri wa kuzalisha wachezaji wenye
ubora na viwango na kwamba njia moja ya msingi ni kuwa na mashindano ya
ngazi za chini hasa mashuleni"Alisema Twissa
Amesema vifaa
walivyovitoa ni sehemu ya Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali za
kutekeleza mikakati ya uzalishaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na
kwamba Vodacom inafurahia mpango huo.
Mashindno hayo
maalum yataratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa – BMT na kwamba
utaratibu umewekwa wa kuapat sekondari 12 kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa
Dar es salaam ambapo kila Wilaya itatoa sekondari 4.