Saturday, September 14, 2013

PICHA TOFAUTI::HIVI NDIVYO MAYWEATHER ALIVYOMCHAKAZA MMEXICO USIKU WA KUAMKIA LEO



Bondia Mayweather ameendeleza rekodi ya kucheza mapambano 46 bila ya kupoteza hata moja huku akiwa ameshinda 26 kwa KO.
Mayweather ambaye aliingia ulingoni akisindikizwa na rafiki yake Li Wayne alionyesha uwezo mkubwa ingawa mpinzani wake hakuwa laini.

Leo asubuhi, Mayweather amefanikiwa kumshinda Saul Alvarez wa Mexico ambaye kabla alikuwa hajapoteza pambano hata moja.

Jaji wa kwanza alitoa sare ya pointi 114-114, lakini wawili wakatoa ushindi kwa Mayweather kwa pointi 116-112, 117-111.
Mayweather alitawala karibia raundi zote kuanzia ya tatu akipiga ngumi moja moja za kudokoa ambazo zilimzidi Mmexico huyo.
Kwa upande wa raundi, Mayweather alishinda kila raundi kuanzia ya kwanza hadi ya 12.

Alvarez alionyesha uwezo kwa kupambana hadi mwisho, hata hivyo Mayweather alionyesha ni bora zaidi yake kiufundi.
Namna alivyokuwa anakwepa na kupiga, alimpa wakati mgumu Alvarez ambaye pia alionyesha atakuwa tishio zaidi.

Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza la Alvarez kupoteza baada ya kucheza mapambano zaidi ya 40, huku Mayweather akiendelea na rekodi ya kutopoteza.
 Still champion: Floyd Mayweather was hugely impressive in beating Saul Alvarez over 12 rounds in Las Vegas