
Sehemu ya pili ya mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku wa jana kwa michezo nane iliyopigwa kwenye miji mikuu ya soka barani humo .
Kwenye uwanja wa Nou Camp Fc Barcelona waliwafunga Ajax Amsterdam 4-1 huku Lioneln Messi akiwa nyota wa mchezo baada ya kumjibu Cristiano Ronaldo kwa kufunga mabao matatu pekee yake . Bao lingine la mchezo huo lilifungwa na beki Gerrard Pique .


Jijini Milan kwenye uwanja wa Giuseppe De Meazza Ac Milan walipata ushindi wa tabu wakiwafunga Glasgow Celtic 2-0 . Wafungaji wa Milan kwenye mchezo huo walikuwa Sulley Muntari na Cristian Zappata .

Katika matokeo yaliyoshangaza wengi usiku wa jana (Jumatano) mabingwa wa zamani wa amshindano haya Chelsea The Blues walipoteza mchezo wao dhidi ya Fc Basle tena kwenye uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge . Basle walishinda kwa mabao mawili kwa moja wafungaji wakiwa Marco Streller na Mohamed Salah huku Chelsea wakifunga kupitia kwa Oscar.

Arsenal waliendeleza mwanzo mzuri kwa timu za England kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa baada ya kuwafunga Olympique Marseille kwa mabao mawili kwa moja . Mabo ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Aaron Ramsey huku Marseile wakifunga kupitia kwa Jordan Ayew ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati.
Mechi iliyokuwa inatazamiwa na wengi kuwa mechi ngumu pengine kuliko mechi zote za jana iliwakutanisha washindi wa pili wa ligi za Italia na Bundesliga Napoli na Borrusia Dortmund . Katika mchezo huo uliopigwa huko Italia Napoli walishinda kwa mabao mawili kwa moja. Wafungaji wa Napoli walikuwa Gonzalo Higuain na Lorenzo Insigne huku Camilo Zuniga wa Napoli akijifunga mwenyewe kuipa Dortmund bao pekee lao mchezo huo .
Timu nyingine toka Hispania Atletico Madrid ilishinda mchezo wao dhidi ya Zenith St Petesburg kwa matokeo ya 3-1 huku Schalke 04 nao wakishinda mchezo wao dhidi ya Steua Bucharest kwa 3-0 . Nao Fc Porto waliwafunga Austria Wien 1-0.
Matokeo ya UEFA Champions League.
Fc Barcelona 4-0 Ajax Amsterdam.
Ac Milan 2-0 Glasgow Celtic .
Napoli 2-1 Borrusia Dortmund.
Marseile 1-2 Arsenal.
Chelsea 1-2 Fc Basle.
Atletico Madrid 3-1 Zenith St Petersburg.
Austria Vienna 0-1 Fc Porto.
Schalke 04 3-0 Steua Bucharest.