Wednesday, September 11, 2013

GARI LA WAGONJWA (AMBULACE) LATUMIKA KATIKA WIZI WA MAFUTA HUKO GEITA KATIKA MGODI WA DHAHABU

9
Mwandishi wa habari Denice Stephano anakwambia hii ishu imefanya wapatikane watuhumiwa tisa wa kesi ya wizi wa mafuta katika mgodi wa Dhahabu ( GEITA GOLD MINE ) kwa kutumia gari la wagonjwa (Ambulance) ambapo wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka matatu.



Mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Abiner ameiambia mahakama September 9 2013 kwamba 5/09/2013 saa 7:30 usiku uko eneo la Geita power ndani ya mgodi wa Geita gold mine watuhumiwa waliiba mafuta lita 630 ya dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo na kuharibu mali ambayo ni gari la kubeba wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwa kuling’oa viti



Mtuhumiwa wa kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari anatuhumiwa makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya gari.


1Abiner ameongeza kuwa washitakiwa hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba za usajili T 671 AKW mali ya Halmashauri ya wilaya ya Geita  na kuingia mgodini kuiba mafuta aina ya Diesel lita 630 yenye thamani ya Tsh. 1,386,000/= mali ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)  


Waliofikishwa mahakamani ni Hamudi Biembo dereva wa gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31)  mkazi wa mtaa wa  Mseto Geita,Selemani Magoso (31 )ambaye ni dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa Shilabela Geita, Julias Boazi (28) mkazi wa Msalala road Geita )Wengine ni Rashid Hussen (27) Mlizi wa mgodi, Ismail Zuber (26)mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) Operator wa GGM