
Baada
ya Black Rhyno kutangaza kupata mtoto wa kike jana, huyu tena ni
mwanafamilia mwingine wa muziki wa Tanzania aliyetangaza kupata mtoto wa
kiume. Mwanafamilia huyu sio mwingine bali ni
Babu Tale ambaye ni meneja wa kundi la Tiptop Connection. Kupitia
ukurasa wake wa Instagram ameandika “My new kaka. Asante mungu”. Pongezi
nyingi kwake na familia yake.
