Thursday, September 19, 2013

DIVA WA CLOUDZ FM AMSHUTUMU Mh. ZITO KWA KOSA LA KUTOMSHUKURU KWA IDEA YA KIGOMA ALL STAR EAST AFRICA TOUR

 


Stori: Jelard Lucas
MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness  Malinzi ‘Diva’ amesema alichokuwa anahitaji katika sakata lake la kudai ameibiwa ‘idea’ ya Kigoma All Star East Africa Tour na Mhe. Zitto Kabwe ni kupewa heshima yake (appreciation) tu.
Mhe. Zitto Kabwe.
Katika maelezo yake, Diva amefunguka kuwa walijadili na Zitto kuhusu idea hiyo lakini badala yake akashangaa mheshimiwa anampotezea katika utekelezaji kitu ambacho anadai siyo ‘feya’
“Angalau basi angenitaja kama kunishukuru kwa kutoa mchango wangu katika Kigoma All Star Tour lakini hakufanya hivyo na hata nilipomsisitiza aliniletea siasa,” alisema Diva.
Jitihada za kumpata Zitto hazikuzaa matunda ila tunaendelea kumsaka.