
Bingwa
wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya
kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa
Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda
shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi
sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani
baada ya
kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.
“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo
hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee
na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine “.Habari kamili ipo kwenye
gazeti la Mwananchi la Sept 17.