TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili nchini jana mchana kwa ziara ya kikazi katika Tanzania ambako baadaye atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam, Mheshimiwa Rajoelina amepokelewa na mwenyewe wake, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC-Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais Kikwete ndiye amepewa jukumu na viongozi

wenzake wa nchi wanachama wa SADC kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa katika Kisiwa cha Madagascar.
Viongozi hao wawili watakutana Ikulu, Dar es Salaam baadaye leo kuzungumzia hali ya kisiasa nchini Madagascar ambako Rais Kikwete atamweleza Mheshimiwa Rajoelina kuhusu matokeo ya kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Asasi (SADC-Troika-Summit) kilichofanyika chini ya uenyekiti wake juzi, Jumamosi usiku, mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Naye Raojelina anatarajiwa kumwelezea Rais Kikwete kuhusu hali ilivyo katika Madagascar na hasa kuhusiana na jitihada za kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini ambao umekuwa unakumbwa na changamoto kadhaa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Julai, 2013

Rais Kikwete na Rais Rajoelina wazungumza kwa marefu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina jioni ya jana, Jumatatu, Julai 22, 2013 wamekutana kwa mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mgogoro wa kisiasa katika Madagascar na njia za kuweza kutoka katika mgogoro huo.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam yaliendelea kwa zaidi ya dakika 75 na Mheshimiwa Rajoelina alimweleza Rais Kikwete kuhusu hali ya kisiasa ilivyo katika Madagascar na kuomba ushauri kutoka kwa Mheshimiwa Kikwete kuhusu jinsi gani ya kukabiliana na hali hiyo.
Rais Rajoelina amemwambia Rais Kikwete mwanzoni mwa mazungumzo hayo:“Mheshimiwa Rais, nianze kwa kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu kwa kuwa binadamu ambaye umetusikiliza sana. Tunakushukuru sana kwa juhudi zako na ari yako binafsi kujaribu kufanikisha zoezi la kuitoa Madagascar katika kipindi inachopitia. Ni wakati wa shida, kama huu kwetu, unapopata kujua marafiki wa kwelikweli. Kwahakika, Mheshimiwa Rais, umekuwa rafiki halisi wa nchi yetu.”
Rais Kikwete naye alitumia muda kumweleza Mheshimiwa Rajoelina jinsi Tanzania, nchi nyingine na taasisi nyingine muhimu za kisiasa duniani, ikiwamo Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuia ya Ulaya(EU) zinavyoina hali ya Madagascar na njia zipi zinaweza kutumika kukitoa Kisiwa hicho kikubwa kuliko vyote katika Afrika katika mgogoro wa sasa.
Viongozi hao wawili wamekubaliana kukutana tena asubuhi ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013, kuendelea na mazungumzo kwa nia ya kupata majawabu ya kwelikweli na yanayoweza kukubalika kwa pande zote zinazovutana katika Madagascar kuhusu jinsi gani ya kuitoa nchi hiyo katika matatizo yake ya sasa.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika-Organ) yaSADC ndiye amepewa jukumu na viongozi wenzake wa SADC kutafuta majawabu katika migogoro ya kisiasa inayozikabili nchi wanachama wa SADC ikiwamo Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Zimbabwe.
Mheshimiwa Kikwete amekuwa anahangaika na mzozo wa Madagascar na mara tatu amemwalika Rais Rajoelina kuja nchini kwa mazungumzo yenye lengo la kumaliza mgogoro katika nchi hiyo.
Mapema jana mchana, Rais Kikwete amempokea Rais Rajoelina na ujumbe wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa mazungumzo ya baadaye jioni.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.