MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dodoma Mjini, jana ilimuachia huru Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (41), maarufu kama Sugu aliyefikishwa
mahakamani kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu
Mizengo Pinda baada ya hati ya mashtaka kuonesha mapungufu.
Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama imeutaka upande wa mashtaka
kurekebisha hati hiyo na kumfikisha tena mshtakiwa mahakamani huku
Wakili wa Mbilinyi, Tundu Lissu akitaka kesi mpya itakayoletwa
mahakamani iwe na maelezo ya Waziri Mkuu na awe tayari kusimama
mahakamani kuthibitisha shitaka hilo.
Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Elinaza Luvanda.
Awali akimsomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Harriet
Lopa alidai kuwa Juni 24, mwaka huu, Mbilinyi akiwa Dodoma alituma
ujumbe wenye lugha ya matusi kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook
kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mshtakiwa alikana shitaka hilo. Hata hivyo wakili wa Mshtakiwa, Lissu
aliomba kutoa hoja na kusema hati ya mashtaka ni mbovu na kuomba
Mahakama itupilie mbali kwa sababu ina makosa.
“Lugha ya matusi haikutajwa, lugha gani hiyo ya matusi na hati ya
mashtaka iko kimya, mshtakiwa atajitetea vipi,ataandaa utetezi namna
gani kwani hata kinachodaiwa kuwekwa kwenye facebook hakijasemwa,”
alidai Lissu.
Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali alisema kesi hiyo bado iko
kwenye upelelezi na kutaka mshtakiwa aendelee na mashtaka yake mpaka
itakapothibitishwa vinginevyo.
Kutokana na kauli hiyo ya wakili wa Serikali, Lissu alizidi
kusisitiza hati ya mashtaka haina maelezo ya kutosha na inatakiwa
kukidhi matakwa ya sheria.
“Hati ya mashtaka iliyoletwa si halali kinyume na kifungu cha 132 cha
mwenendo wa makosa ya jinai na itakuwa makosa kama Mahakama ikikubali
hati hiyo,” alisema.
Alitoa uamuzi wa Mahakama, Hakimu Luvanda alisema anakubaliana na
maelezo ya Wakili upande wa utetezi Lissu kuwa hati hiyo ina mapungufu.
Alisema Mahakama inamuachia huru mshtakiwa na upande wa mashtaka
unaweza kumshtaki tena mshtakiwa kama itaona umuhimu wa kufanya hivyo.
Akizungumza nje ya Mahakama Lissu alisema hati ya mashtaka dhidi ya
Mbilinyi kuwa alitoa lugha ya matusi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
haijaeleza anachodaiwa kusema Mbilinyi.
Alisema Mahakama imetenda sawasawa kuifuta hati hiyo ilitakiwa
ifafanue lugha ya matusi iliyotumika ni ipi. ”Hakimu hajasema Sugu hana
makosa, lakini upande wa mashtaka ukajipange kutengeneza hati mpya,”
alisema.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imetupilia
mbali mashitaka yaliyokuwa yamefunguliwa na serikali dhidi ya Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kwa madai ya kumtukana Waziri
Mkuu Mizengo Pinda.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Eliezel Luvanda
alitupilia mbali mashitaka hayo kutokana na hati ya mashitaka dhidi ya
mbunge huyo kuwa na upungufu.
Luvanda alisema kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20) hati hiyo
haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani iliyodaiwa kuwa
ni ya matusi aliyotumia mshitakiwa huyo dhidi ya Pinda.
Awali akisoma hati hiyo, Mwendesha Mashitaka, Hariet Lopa alidai kuwa
Juni 24 mwaka huu akiwa katika Manispaa ya Dodoma, Mbilinyi aliweka
ujumbe wenye lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu Pinda kinyume cha
sheria.
Kabla ya hakimu kutoa hukumu hiyo, wakili na mwanasheria wa CHADEMA,
Tundu Lisu, aliwasilisha utetezi wake mbele ya mahakama hiyo akiitaka
kuitupilia mbali kesi hiyo kwa vile hakuna matusi yanayotajwa yakidaiwa
kutolewa na mbunge huyo dhidi ya Pinda.
Lissu alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20), hati
hiyo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani
iliyotumika na ni matusi gani, hivyo haiwezi kuwa kesi ambayo inaweza
kuendelea kusikilizwa.
Lissu alidai kuwa maneno yanayodaiwa yangesababisha uvunjifu wa amani
hayakutajwa katika hati hiyo huku akihoji upande wa mashitaka unataka
Sugu ajitetee kwa shitaka lipi.
Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa kama hati hiyo ya mashitaka
iliyopelekwa mahakamani hapo itaendelea kutumika, itakuwa imekiuka
sheria, hivyo akaitaka mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.
Hakimu Luvanda alipomtaka mwendesha mashitaka wa serikali kujibu hoja ya
Lissu, alishikilia msimamo wake na kuiomba mahakama kuendelea
kuisikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa ni mpya, hivyo makosa ambayo yapo
yatafanyiwa marekebisho wakati shauri likiendelea.
Hata hivyo Lissu alipinga kauli ya mwanasheria wa serikali kwa madai
kuwa hati ya mashitaka ni chafu na imeandaliwa ovyo, hivyo mahakama
kukubali kuendelea kusikiliza kesi hiyo ni kosa na hivyo ni vyema
ikatupiliwa mbali.
“Mheshimiwa hakimu naomba kesi hii itupiliwe mbali kwa kuwa hati ya
mashitaka ni chafu na ni ya ovyo. Naomba itupiliwe mbali na mtuhumiwa
aachiwe huru,” alisema Lissu na kuongeza kuwa wapo tayari hata kesho
kuendelea na kesi hiyo ikiwa serikali itaandaa hati sahihi.
Hata hivyo, baada ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka
alidai wataendelea na upelelezi na ukikamilika wataandaa hati mpya.
Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, Lissu alisema mahakama hiyo
imetenda haki na kama upande wa mashitaka haukuwa umeridhika na hukumu
hiyo, ujipange upya na kupeleka hati ya mashitaka.
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) alisema hata
hivyo kufutwa kwa kesi hiyo hakumaanishi mteja wake hawezi kushitakiwa
tena, kwani bado Waziri Mkuu Pinda anaweza kwenda polisi kutoa maelezo
kama anaona kweli ametendewa kosa hilo.
Kwa upande wake, Sugu baada ya kuachiwa huru alisema kuwa anachoshauri
ni Pinda kujitafakari upya juu ya kauli zake anazozitoa hasa kuhamasisha
watu kupigwa.
Awali, Sugu alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma kuwa
aliweka ujumbe mfupi katika mtandao wa kijamii ambao ulikuwa unamtusi
Waziri Mkuu Pinda.
Hata hivyo, alikuwa akipelekwa katika kituo cha polisi cha kati kwa
mahojiano na jana ilikuwa ni mara ya kwanza kufikishwa mahakamani
- See more at: http://kariakoodsm.blogspot.com/2013/06/sugu-ambwaga-pinda.html#sthash.LeAiO4F8.bnKoc1Do.dpuf