SERIKALI imesisitiza kuwa itaendelea kuwashughulikia watu wote
wanaosababisha vurugu, fujo na kukaidi sheria za nchi.
Uamuzi huo wa
serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na
Uratibu), Stephen Wassira, alipokuwa akifanya majumuisho ya mjadala wa
hotuba ya mipango ya maendeleo ya serikali kwa mwaka 2013/14, aliyoitoa
wiki mbili zilizopita, bungeni mjini hapa jana.
Alisema amani ni muhimu katika taifa lolote ili liweze kupata maendeleo. “Amani ikikosekana hakuna maendeleo na kama hakuna maendeleo hakuna amani,” alisema.
Alisema amani ni muhimu katika taifa lolote ili liweze kupata maendeleo. “Amani ikikosekana hakuna maendeleo na kama hakuna maendeleo hakuna amani,” alisema.
Wassira aliunga mkono matamshi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni Alhamisi iliyopita, kuwa serikali haitakuwa na msamaha kwa watu wanaovuruga amani, utulivu na kusababisha ghasia na vurugu nchini.
Alisema viongozi wote nchini hasa wanasiasa, wana dhamana kubwa ya kuhakikisha amani inadumishwa na kujenga demokrasia ya kweli ya kushindana kwa hoja.
“Hatuwezi kuruhusu nchi yetu iwe ya majaribio ya vurugu na fujo. Tushindane kwa hoja, fujo haiwezi kuwa hoja. Ni kifungu kipi cha Katiba ya nchi kinachoruhusu watu kukaidi sheria. Tusijifiche katika haki za binadamu… ni demokrasia gani ya kuandamana na kukanyaga nyanya zangu,” alisema Wassira
Alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, ikivurugika watu wote wataathirika wakiwamo wanasiasa, hivyo akawataka viongozi wa kisiasa kuacha ushabiki wa vyama katika mambo ya kitaifa na ujenzi wa demokrasia ya kweli nchini.
Wakati huo huo, Jaji mstaafu, Mark Bomani, ameishambulia Serikali na Jeshi la Polisi kuwa wanatumia nguvu kubwa kukabiliana na umma kwa silaha za moto, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watu na taifa.
Amesema nchi ipo katika hali ya sintofahamu, kutokana na matukio yanayotokea yakiwa na ishara za ugaidi, huku Serikali ikiendelea kuwa kimya ikiwaacha baadhi ya raia na viongozi wa vyama vya siasa wakilumbana pasipo kuwachukulia hatua.
Jaji Bomani alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza katika Kongamano la mwaka la maadili ya waandishi wa habari Tanzania, lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Alisema utendaji wa Jeshi la Polisi ni wa kutiliwa shaka na upo wasiwasi wa iwapo wanazijua sheria zinazoelekeza namna ya matumizi ya silaha za moto.
Alitaja kifungu cha sheria sura 223 (4), kinachozuia mtu yeyote kumiliki silaha hata kama ana haki ya kuimiliki na kutembea nayo popote na kuitumia pasipo ruksa.
“Nadhani hao askari hawana uelewa mzuri wa sheria kuhusu silaha za moto, bali wanafanya kazi kwa kuagizwa, kama wangejua sheria wasingejaribu kuzitumia kupambana na raia.
“Kitu kibaya zaidi ni pale kiongozi wa Serikali anapotoa kibali kwao cha kupiga, inawezekana kabisa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alitoa kauli hiyo akiwa na maana fulani, lakini askari wetu hawa hawana uelewa wa uchambuzi wa kauli,” alisema Jaji Bomani.
Alisisitiza kuwa silaha za moto zinaruhusiwa kutumiwa na maofisa usalama wa taifa au wa polisi pale tu panapotokea mtuhumiwa kujaribu kutoroka au wakati nchi ikiwa katika hali ya hatari.
“Hali hii ikiachwa hivi hivi taifa hili halitafika, ingawa tuna safari ndefu kuendeleza amani, upendo na mshikamano, enzi za Mwalimu Julius Nyerere alitangaza maadui watatu, umasikini, maradhi na ujinga lakini kutokana na mabadiliko ya uongozi, watu kwa kujiamulia wameongeza maadui wengine.
Gesi Mtwara
Akizungumzia mvutano wa gesi kusafirishwa kwa bomba kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, alisema wananchi walikuwa na haki ya kuzuia, kwa sababu hawakuwa na elimu yoyote juu ya rasilimali hiyo.
Alisema kiini cha mvutano wa gesi Mtwara ni kutokuwa na taarifa sahihi kutoka serikalini ambayo ilipaswa kutolewa kwa wananchi au kwa waandishi wa habari.
“Athari zote zilizotokea zinapaswa kubebwa na Serikali kwa kushindwa kutoa taarifa sahihi, naomba niulize kwamba, juzi nimeshuhudia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini na makampuni makubwa duniani, kuzalisha umeme wa megawati 400 pale Mtwara na kuusambaza Songea, je nani kalalamika?
“Hivyo Serikali inapaswa kujua kwamba, kama ingetoa elimu kwa wananchi juu ya mpango wao, yasingetokea hayo na kuyahusisha na masuala ya kisiasa,” alisema.
Aidha, katika hatua nyingine, Jaji Bomani alikumbusha suala la maadili ya waandishi wa habari kwa kueleza kuwa tasnia hiyo ni mhimili wa nne wa dola, hivyo waandishi lazima wawe na msimamo madhubuti ili kuheshimiana kati yake na Serikali.
Jaji Bomani alisema, tasnia ya habari ikiwa na msimamo na kutotumiwa itaifanya Serikali kutekeleza wajibu wake kwa kuhofia waandishi watawajuza wananchi ambao wana uwezo wa kuchukua maamuzi halali.
“Juu ya upotevu wa amani kwa waandishi wa habari, nasema mtajikomboa kwa kujisimamia wenyewe na kupinga kudhibitiwa na dola, kwani inawatazama kwa jicho jingine hivyo basi lazima kuwepo na elimu ya kutosha ya uchambuzi wa kina,” alisema.
Pamoja na mambo mengine alizindua kitabu maalum cha mwongozo wa maadili ya waandishi wa habari na kuwataka wamiliki wa vyuo kukitumia.