Monday, June 24, 2013

RATIBA KAMILI YA UJIO WA RAIS OBAMA ATAKAPO ZULU TANZANI


Ikulu ya Marekani na Idara ya Habari maelezo ya Rais wa (Maelezo) Tanzania wametangaza rasmi ratiba
ya Rais Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha atakaa kwa
siku mbili tu kuanzia Julai 1 na kuondoka Julai 2, mwaka huu.
Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya
Senegal na Afrika Kusini. Atatua Senegal keshokutwa.
Mara atakapowasili Julai 1 na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais
Obama atazindua barabara mpya katika upande wa mashariki wa geti la
kuingia Ikulu.
Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe Michelle pia siku hiyo ya Julai 1,
pia atazungumza kwa nyakati tofauti na  kundi la wafanyabiashara kutoka
nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam.
"Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania," ilisema taarifa ya Maelezo.
Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria dhifa ya taifa
atakayoandaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake Rais Jakaya
Kikwete.
Siku inayofuata Rais Obama ataweka shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa
Ubalozi wa Marekani kama kumbukumbu ya watu waliofariki kufuatia
shambulizi la kigaidi la bomu lililofanyikwa mwaka 1998.
Watu 11 walifariki na 85 kujeruhiwa kufuatia shambulizi hilo ambalo
lilifanywa siku moja na Ubalozi wa Marekani nchini Kenya.
Rais Obama pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion
na atatoa hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia bara la
Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
"Tanzania ni mshirika muhimu wa Marekani," anasema Ofisa wa Ikulu ya
Marekani, Ben Rhodes wakati alipozungumza na waandishi wa habari
wikiendi iliyopita kwenye Ikulu ya Marekani jijini Washington kuhusu
ratiba ya ziara ya Obama barani Afrika.
"Tanzania ni washirika wetu katika masuala mbalimbali ya usalama kwenye
ukanda wa Afrika Mashariki. Pia tunasaidia katika miradi mingi na
tunaiona kama nchi yenye utawala bora," amesema Rhodes, ambaye pia ni
msemaji wa Baraza la Usalama la Marekani.
Pia mke wa Obama atakuwa na ratiba yake, ambapo atapata staftahi na
mwenyeji wake Mama Salma Kikwete, Julai 1 katika ofisi za Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo (Wama) jijini Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ubalozi wa zamani wa Marekanio na baadae
atashuhudia onyesha la utamadunia la Kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho
kinajumuiosha watoto wa mitaani wenye umri kuanzia miaka mitano hadi 18
kwenye Makumbusho ya Taifa.
Mama Obama amepangiwa Julai 2, kuhudhuria mkutano na wake wa marais wa
nchi za Afrika.
Laura Bush, ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa Marekani, pia atahudhuria
mkutano huo wenye lengo la kuunga mkono jitihada za kuwakomboa kiuchumi
wanawake wa Afrika.