Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mabalozi wateule wa
Tanzania, wanaokwenda kuripoti kwenye Vituo vyao vya kazi nje ya nchi,
wakati mabalozi hao walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es
Salaam, leo Juni 19, 2013 kwa ajili ya kumuaga mhe. Makamu. Kutoka
Kushoto ni Balozi Modest Mero, anayekwenda Umoja wa Mataifa, Geneva,
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, anayekwenda, Abu Dhabi UAE, Balozi
Chabaka Kilumanga, anayekwenda Comoro, Balozi Wilson Masilingi,
anayekwenda The Hague, Uholanzi na Balozi Liberata Mulamula, anayekwenda
Washington D.C, Marekani.