Wednesday, June 26, 2013

JUMA KASEJA ATEMWA 'KIROHO MBAYA' SIMBA SC

MLINDA mlango nambari moja Tanzania, Juma Kaseja Juma amehitimisha miaka yake tisa ya kuitumikia klabu ya Simba SC baada ya klabu hiyo kuamua kutomuongezea Mkataba, baada ya Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Habari ambazo share imezipata kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba Kaseja anaachwa baada ya kuitumikia kwa mafanikio makubwa klabu hiyo tangu mwaka 2003 aliposajiliwa kutoka Moro United, eti kwa sababu hakubaliki kwa sasa na wapenzi wa timu hiyo.
Hata hivyo, jambo la kusikitisha tu ni kwamba hakuna sababu za msingi za kuachwa kwa mlinda mlango huyo, zaidi tu ya kuonekana wamemchoka baada ya kuwa naye kwa muda mrefu.