BREAKING NEWSSSS MAWAZIRI WATACHUJWA KUMPOKEA OBAMA PIA WAFANYA KAZI WA UWANJA WA NDEGE WAPEWA LIKIZO YA SIKU MBILI
wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wapewa likizo ya siku 2 kila kitu kitafanya na wamarekani ikiwapo kukagua wasafiri.
mawaziri watachujwa kumpokea Obama watatajwa na wamarekani wenyewe.
Dar es Salaam. Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack
Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa
kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki
aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni
kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.
Pia
alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu
saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika
majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa
abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa
siku mbili.
“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia
wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,”
alisema Malaki.
Aliongeza kuwa japokuwa Mamlaka ya Anga
Tanzania (TAA) inaendelea kufanya kazi zake kama kawaida, lakini
Jumatatu, Wamarekani watasimamia kila kitu hadi ukaguzi wa wageni.
“Siku hiyo mwongoza ndege wa TAA, atafanya shughuli kidogo, mambo mengine yatafanywa na wao,” alisema.
Idadi ya maofisa wa Tanzania
Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.
“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo
katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:
“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais
Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”
Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri
wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache
watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza
majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.
“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chikawe.